Wafuasi wa falsafa ya Thomas Sankara ya Afrika kwanza na kujitegemea, bado wanamasikitiko wakati nchi ikisimaisha tena kumbukumbu ya Sankara.
Luc Damiba katibu wa kamati ya kimataifa ya kumbukumbu ya Thomas Sankara, alikosoa vikali maombi ya msamaha ya rais wa zamani wa Burkina Faso, Blaise Compaore ya Jumanne.
Damiba anasema Compaore anafanya hivyo kuchezea vichwa vya watu, lengo la lake ni kurejea Burkina Faso na kupata msamaha wa rais.
Rais huyo wa zamani wa Burkina Faso, aliyehukumiwa kifungo cha maisha kipindi akiwa uhamishoni kwa kuhusika na mauaji ya mwaka 1987 ya kiongozi nembo ya mapinduzi Thomas Sankara, Jumanne aliomba radhi kwa familia ya Thomas Sankara.
Katika ujumbe ambao ulisomwa na msemaji wa serekali Lionel Bilgo, Compaore amesema “nawaomba msamaha watu wa Burkina Faso kwa matendo yangu yote ambayo niliyafanya wakati nikiwa madarakani hasa familia ya kaka yangu Thomas Sankara.”