Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 06:15

Wafilipino wapinga matokeo ya uchaguzi wa rais


Waandamanaji wanaopinga matokeo yasiyo rasmi ya uchaguzi wa rais, wakusanyika Manila.
Waandamanaji wanaopinga matokeo yasiyo rasmi ya uchaguzi wa rais, wakusanyika Manila.

Marcos Junior anaefahamika zaidi kwa jina la Bongbong, amepata asili mia 56 za kura, huku mpinzani wake mkuu, makamu rais Leni Roberdo akitoa wito wa umoja na utulivu kwa wafusai wake.

Mgombea huyo alipata kura milioni 30.8 sawa na asili mia 56, ikiwa ni mara mbili zaidi ya mpinzani wake mkuu, mtetea haki za binadamu Leni Roberdo aliyepata kura milioni 14.7, ikiwa asili mia 97 za kura zimekwisha hesabiwa kufikia jioni ya Jumanne saa za Ufilipino.

“Watu wamepokea vizuri ujumbe wetu wa umoja kotoke unakokwenda. Kwa sababu wafilipino wanaamini hiyo ndio hatua yetu ya kwanza kurudi kwenye maisha ya kawaida na kuimarisha maisha ywtu sote,” amesema Marcos Jr.

Robredo ambae ndiye makamu rais kwa hivi sasa alitowa wito kwa wafuasi wake kuwa watulivu wakati walipoanza maadamano kupinga matokeo hayo, ambayo anadai yalikua na kasoro.

Nina fahamu munaipenda nchi yetu, lakini upendo huu usisababishe kugawanyika kwetu sisi. Hata ikiwa kuna kura zinazoendelea kuhesabiwa na hata ikiwa kuna hoja kuhusu kasoro kwenye uchaguzi, nina omba tusikilize sauti ya wananchi na tuwe pamoja,” amesema Robredo.

Wafuasi wa Robredo wana hofu na kueleza usikitifu kutokana na kushindwa kwa mgombea wao lakini wanasema wataendelea na upinzani wao.

Mimi nina hofu na nina usikitifu mkubwa sana kwa jambo hili linatendeka nchini mwangu. Sikudhani maishani mwangu yote nitashuhudia kurudi kwa utawala mwengine wa Marcos. Kwa hakika inavunja moyo,” amesema KC, mfuasi wa Robredo

Ushindi wa Marcos Junior ni pigo kwa mamilion ya wafilipino ambao walitaraji kubadili muelekeo wa nchi yao baada ya miaka 6 ya utawala wa kimabavu chini ya rais anaeondoka Rodrigo Duterte.

Na zaidi ya hayo baadala kupinga ukiukaji mkubwa ulotokea chini ya Duterte, wapiga kura wa Ufilipino walimpatia ushindi mkubwa binti yake Sara, kwenye uchaguzi wa makamu rais.

Kiongozi wa maandamano Renato Reyes Jr anasema kwamba maandamano yana lengo la kueleza hasira na chuki za wananchi.

Renato Reyes Jr, kiongozi wa maandamano

Watu hawajakubali kushindwa. Si dhani watakubali kamwe kusindwa na wako hapa kueleza hasira zao kutokana na mfumo wa kisiasa uloruhusu familia ya dikteta Marcos kurudi madarakani kama rais,” amesema Reyes.

Marcos Junior, mwenye umri wa miaka 50 amekata katu wakati wa kampeni zake, kulaani ukatili na ulaji rushwa ulokua ukiendelea chini ya utawala wa babake mnamo miaka ya 1980, akipinga tuhuma kwamba familia yake imeiba karibu dola bilioni 10 ilipokua madarakani.

Babake na familia yake walilazimika kukimbia nje ya nchi mwaka 1986, kufuatia mapinduzi ya wananchi.

Mshindi rasmi wa uchaguzi anatarajiwa kuchukua madaraka June 30 kwa mhula mmoja wa miaka 6, na wachambuzi wanasema kunahitajika kipindi cha kutafakari juu ya kuendelea na kampeni ya kudai utawala bora baada ya watoto wa familia mbili zilizokua na utawala wa kimabavu kuchukua tena uwongozi wa taifa hilo la kusini mashariki mwa Asia.

XS
SM
MD
LG