Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 25, 2024 Local time: 16:52

68 wafariki katika ajali ya ndege


Takriban watu 68 wamepoteza maisha Jumapili katika ajali ya ndege iliyotokea Pokhara, Nepal, kwa mujibu wa mamlaka ya anga ya nchini humo, ikiwa ni ajali mbaya katika miongo mitatu iliyopita katika taifa hilo dogo kwenye eneo la  milima ya Himalaya.

Mamia ya wafanyakazi wa uokozi walipelekwa katika eneo la milima ambapo ndege ya shirika la Yeti, iliyokuwa imebeba watu 72 kuanguka ikitokea mji mkuu wa Kathmandu.

Televisheni ya nchini humo imeonyesha wafanyakazi wa uokozi wakiwa wamekusanyika kuzunguka vipande vya ndege iliyoanguka.

Katika baadhi ya enei la tukio moto ulionenaka ukiendelea ukuwaka.

Ajali hiyo imekuwa mbaya zaidi toka mwaka 1992, kwa mujibu wa taarifa za mtandao wa usalama wa usafiri wa anga, ambapo ndege ya shirika la Pakistan International, Airbus 300 ilipo anguka katika vilima wakati ikitua Kathmandu na kuua watu 167 waliokuwemo

XS
SM
MD
LG