Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 28, 2025 Local time: 05:59

Wafanyakazi wa viwanda vya nguo wafanya mgomo Bangladesh


Waandamanaji kutoka viwanda vya kutengeneza nguo wakiwa kwenye barabara za mji wa Dhaka, Bangladesh Alhamisi.
Waandamanaji kutoka viwanda vya kutengeneza nguo wakiwa kwenye barabara za mji wa Dhaka, Bangladesh Alhamisi.

Maafisa pamoja na mashuhuda wamesema kwamba polisi wa Bangladesh Alhamisi wamelazimika kutumia risasi za mipira na gesi ya kutoa machozi kuwatawanya wafanyakazi wa viwanda vya kutengeneza nguo ambao wanapinga nyongeza ya mishahara iliyotolewa na serikali.

Jopo maalum la serikali Jumanne lilitangaza nyongeza ya mishahara ya asilimia 56.25 kwa wafanyakazi takriban milioni 4 wa viwanda vya nguo kwenye taifa hilo la Kusini mwa Asia, ambao walikuwa wakidai nyongeza ya karibu mara tatu ya mishahara yao.

Viwanda 3,500 vya nguo nchini Bangladesh vinachangia takriban asilimia 85 ya dola bilioni 55 zinazopatikana kupitia mauzo ya bidhaa nje ya nchi. Baadhi ya mavazi maarufu yanayotengenezewa huko ni pamoja na Levi, Zara na H&M.

Hali kwa wafanyakazi kwenye sekta hiyo inasemekana kuwa ngumu, wengi wao wakiwa wanawake, wenye mishahara inayoanzia dola 75 za kimarekani kwa mwezi.

Forum

XS
SM
MD
LG