Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 11:08

Wafanyakazi wa Tunisia wagoma kote nchini

Wafanyakazi wa Tunisia katika maandamano ya mgomo.(AP /Hassene Dridi).
Wafanyakazi wa Tunisia katika maandamano ya mgomo.(AP /Hassene Dridi).

Safari za ndege zimesitishwa,usafiri wa umma kusimamishwa na ofisi za serikali kufungwa katika mgomo wa kitaifa uloitishwa na shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini Tunisia Alhamisi, ambao ulipelekea shinikizo kwa rais ambaye tayari anakabiliwa na msururu wa migogoro.

Shirikisho lenye nguvu la wafanyakazi Tunisia UGTT lilitoa wito kwa wanachama wake wapatao milioni tatu wa sekta ya umma kugoma, na kusitisha kazi katika mashirika 159 ya serikali na makampuni ya umma kudai nyongeza za mishahara na kutishia mageuzi.

Kitendo hicho kilionekana kuangaliwa sana. Mgomo wa wafanyikazi wa sekta ya umma katika uwanja wa ndege wa Tunis ulisababisha darzeni ya safari za ndege kufutwa, huku huduma za umma na ofisi za posta zikifungwa.

Takriban watu 1,000 waliogoma walikusanyika nje ya makao makuu ya UGTT katikati mwa Tunis, wakiimba wimbo wa taifa na kupeperusha bendera.

XS
SM
MD
LG