Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 02, 2022 Local time: 11:34

Wafanyakazi wa serikali Afrika kusini wameandamana wakitaka kuongezewa mishahara


wanachama wa muunganio wa wafanyakazi Afrika kuisni COSATU wakiwa wamebeba mabango wakati wa maandamano

Wafanyakazi wa serikali nchini Afrika Kusini wamepanga kuandamana hadi katika wizara ya fedha mjini Pretoria na katika majimbo yote nane ya nchi hiyo, kuishinkiza serikali kuwaongezea mishahara.

Muungano mkubwa wa wafanyakazi nchini humo wa COSATU, na wawakilishi wengine wa zaidi ya wafanyakazi milioni moja wanaofanya kazi katika sekta ya umma, wamewaambia waandishi wa habari kwamba wataendelea kuandamana hadi serikali itakapoongeza mishahara yao zaidi ya pendekezo la asilimia 3 ambayo serikali imetangaza.

Mazungumzo ya nyongeza ya mishahara kati ya miungano ya wafanyakazi na serikali, ilikwama mapema mwezi Oktoba, baada ya serikali kusema kwamba inaweza kuongeza mshahara kwa asilimia 3 pekee iliyowekwa katika bajeti iliyotangazwa katikati mwa mwezi Oktoba.

Muungano wa wafanyakazi wa uma PSA, wenye wanachama 245,000, umesema kwamba serikali haijazingatia matakwa yao yaliyo wasilishwa mapema mwezi huu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG