Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 00:19

Wafanyakazi wa afya Liberia watishia kugoma


wafanyakazi wa afya Liberia wakinyenyua mwili wa mtu anayeshukiwa kuwa na Ebola
wafanyakazi wa afya Liberia wakinyenyua mwili wa mtu anayeshukiwa kuwa na Ebola

Wafanyakazi wa huduma za afya nchini Liberia wanapanga kufanya mgomo kutokana na mgogoro wa malipo hatua ambayo itazorotesha juhudi kubwa za mapambano dhidi ya virusi vya Ebola vinavyosababisha kifo.

Maelfu ya wafanyakazi wa chama cha wafanyakazi wa kitaifa nchini Liberia walisema hawataingia kazini Jumatatu hadi wamepokea nyongeza ya malipo wanayofanya katika kipindi hiki cha ugonjwa hatari wa Ebola.

Wafanyakazi wa chama hicho wanadai dola 700 kwa mwezi nyongeza ya juhudi zao za kufanya kazi katika mazingira hatari ya ugonjwa wa Ebola mbali na mishahara ya mwezi ambayo wanapata kiasi cha dola 200 au dola 300.

Liberia ina idadi kubwa sana ya maambukizo na vifo kutokana na mlipuko mbaya wa ugonjwa wa Ebola. Ugonjwa wa Ebola umeuwa zaidi ya watu 2,300 katika nchi hiyo maskini iliyopo eneo la Afrika magharibi.

Rais Barack Obama
Rais Barack Obama

Wakati huo huo Rais wa Marekani Barack Obama ametoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka ili kuhakikisha mfumo wa huduma za dawa nchini marekani upo tayari kufuata kanuni mbadala za kuwatibu wagonjwa wa Ebola. Rais Obama alizungumza Jumapili na Waziri wa Afya na huduma za jamii nchini Marekani, Sylvia Burwell kuhusu kesi ya kwanza ya maambukizo ya Ebola nchini Marekani.

Bwana Obama aliagiza kitengo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa nchini Marekani-CDC kuchunguza haraka namna muuguzi mmoja katika hospitali ya Texas Health Presbyterian alivyoambukizwa virusi hivyo vya Ebola. Muuguzi huyo alikuwa sehemu ya timu iliyomhudumia Thomas Duncan, mgonjwa wa kwanza kugundulika na Ebola nchini Marekani ambaye alifariki wiki iliyopita.

Maafisa wa afya katika jimbo la Texas wanasema mfanyakazi huyo wa afya alivaa nguo rasmi za kujikinga na kufuata kanuni zilizotolewa na CDC wakati alipomhudumia Duncan.

XS
SM
MD
LG