Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 21, 2023 Local time: 08:11

Wafanyakazi Afrika Kusini kuanza mgomo


Waimbaji wa Afrika Kusini wakati wa fruraha.

Wafanyakazi wa umma Afrika kusini wamekataa mapendekezo ya malipo mapya ya hivi karibuni ya serikali na kusema wataanza mgomo usio na kikomo

Wafanyakazi wa umma Afrika kusini wamekataa mapendekezo ya malipo mapya ya hivi karibuni ya serikali na kusema wataanza mgomo usio na kikomo.

Rais wa chama cha walimu Thobila Ntola aliwaambia waandishi wa habari hii leo kwamba wafanyakazi wanasita kugoma lakini mazungumzo yameshindwa kufikia muafaka kwa mwaka mzima.

Mgomo wa muda mrefu unaeweza kuwa na athari kubwa Afrika kusini nzima . Muungano wa vyama vya wafanyakazi unawakilisha wafanyakazi milioni 1.3 ikiwa ni pamoja na walimu, wafanyakazi wa afya, Polisi na wafanyakazi wengine wa umma.

Vyama hivyo vya wafanyakazi vinataka ongezeko la mishahara la asilimia 8.6 ikiwa zaidi ya mara mbili ya mfumuko wa bei ikiwa ni pamoja na ongezeko la posho ya nyumba.

XS
SM
MD
LG