Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 28, 2023 Local time: 21:36

Waendesha mashtaka Marekani wanataka R.Kelly aongezewe kifungo zaidi


Mwanamuziki R Kelly au Robert Kelly akisindikizwa na polisi kufuatia kesi yake ya picha za ngono

Mumbaji huyo mwenye miaka 56 hatastahili kuachiliwa huru hadi atakapofikisha umri wa miaka 100 iwapo jaji atakubaliana na kifungo cha miaka 25 na ombi jingine la serikali kwamba Kelly aanze kutumikia kifungo chake cha Chicago baada tu ya kifungo cha miaka 30 cha New York kukitumikia kikamilifu

Waendesha mashtaka wa serikali Marekani Alhamisi walimuomba jaji kumpa mwanamuziki R. Kelly kifungo cha miaka 25 zaidi gerezani kwa kosa lake la picha za ngono na ushawishi mwaka jana huko Chicago, ambayo ingeongeza miaka 30 aliyoanza kuhudumu hivi karibuni katika kesi ya New York.

Mumbaji huyo mwenye umri wa miaka 56 hatastahili kuachiliwa huru hadi atakapofikisha umri wa miaka 100 iwapo jaji atakubaliana na kifungo cha miaka 25 na ombi jingine la serikali kwamba Kelly aanze kutumikia kifungo chake cha Chicago baada tu ya kifungo cha miaka 30 cha New York kukitumikia kikamilifu.

Katika mapendekezo yao ya hukumu yaliyowasilishwa kabla ya usiku wa Alhamisi katika Mahakama moja ya Marekani huko Chicago, waendesha mashtaka walielezea tabia ya Kelly kama "ya kikatili", wakimwita "mnyanyasaji wa kingono" asiye na majuto ambaye "ni hatari mkubwa kwa jamii".

"Njia pekee ya kuhakikisha Kelly harudii tena ni kutoa hukumu itakayomweka gerezani kwa maisha yake yote," jalada hilo la serikali lenye kurasa 37 linasema.

Hukumu ya Kelly mjini Chicago imepangwa kutolewa Alhamisi wiki ijayo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG