Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 21:07

Wademokrat wasema wapo tayari kupambana na kinara Donald Trump


Kinara katika mbio za Urais wa Marekani kupitia chama cha Republikan, Donald Trump
Kinara katika mbio za Urais wa Marekani kupitia chama cha Republikan, Donald Trump

Wagombea wawili wa chama cha Demokratic wanaotafuta tiketi ya kugombea urais wa Marekani wamesema wapo tayari kupambana na Donald Trump.

Bi Hillary Clinton na Bernie Sanders, walisema kwamba wako tayari kupambana na mgombea kinara wa tiketi ya chama cha Republikan, Donald Trump, kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Wakizungumza wakati wa mdahalo uliofanyika mjini Flint katika jimbo la Michigan, walisema midahalo yao ni tofauti na ile ya Warepublikan.

Wamedai kwamba siku za hivi karibuni wamekuwa wakishambuliana na kurushiana matusi.

Sanders aliibua kicheko aliposema kwamba Warepublikan wamedhihirisha wazi wazi ni kwa nini utawala wake utalipa kipau mbele swala la kuwekeza kwa taasisi za kushughulikia afya ya akili.

Wakaazi wa mji wa Flint, ambap wengi wao wakiwa ni watu weusi maskini, wamekuwa wakikabiliana na mzozo wa maji yaliyo na kemikali za chuma.

Swala hilo limezua mtafaruku baina ya viongozi wa serikali kwa miezi kadhaa.

Wanasiasa hao wawili, walimtaka Gavana wa jimbo la Michigan, Rick Snyder, kujiuzulu kufuatia kashfa hiyo.

XS
SM
MD
LG