Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 03:52

Wademokrat waonekana kuwa na mvutano katika kupitisha mswaada wa masuala ya kijamii na mazingira

Sen. Joe Manchin, D-W.Va., akizungumza na waandishi wa habari huko bungeni . Nov. 1, 2021.
Sen. Joe Manchin, D-W.Va., akizungumza na waandishi wa habari huko bungeni . Nov. 1, 2021.

Wademokrati  wanaonekana kuwa na mvutano katika kusukuma kupitisha mswaada wa maswala ya kijamii na mazingira kabla ya sikukuu ya Christmas wiki ijayo.

Wademokrati wanaonekana kuwa na mvutano katika kusukuma kupitisha mswaada wa maswala ya kijamii na mazingira kabla ya sikukuu ya Christmas wiki ijayo.

Shirika la Habari la AP na mashirika mengine yaliripoti jana kwamba kutokana na taarifa kutoka kwa watu walio na ujuzi wa mashauriano yanayoendelea, seneta Joe Manchin anazuia kuhusu mpango unaoongeza muda wa program ya kutoa msaada wa fedha za kodi kwa watoto kwa mwaka mmoja, maarufu kama “child tax credit”.

Amewaambia waandishi wa habari jana jumatano kwamba siku zote amekuwa upande wa utoaji wa kodi kwa watoto na kuwa ripoti za upinzani wake kuwaweka katika sheria ni uzushi mkubwa.

Manchin ameeleza upinzani wake katika ukubwa wa program nzima iliyopendekezwa na rais Joe Biden, awali wademokrat walipitisha mpango wa dola bilioni 3.5 kabla ya kupunguza kufikia trilioni 2 kujaribu kurahisisha mpango huo.

Chanzo cha habari hii ni vyanzo mbalimbali ikiwemo Shirika la habari la AP

XS
SM
MD
LG