Maafisa wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC wanasema ajali ya migodi katika eneo moja dogo huko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo imewauwa wachimba madini 60.
Maafisa wa serikali wanasema watu hao walikuwa wakichimba dhahabu kiasi cha mita 100 chini ya ardhi Jumatatu wakati mgodi ulipoporomoka na kuwafukia.
Eneo hilo linapakana na Pangoyi katika jimbo la Orientale. Maafisa wanasema eneo hilo linadhibitiwa na wanamgambo na kwamba wametatiza juhudi za waokozi.
Maelfu ya watu katika nchi hiyo maskini wanajaribu kutafuta riziki zao za kila siku kwa kufanya kazi katika maeneo yasiyo salama ambayo yanahusisha uchimbaji mdogo mdogo wa madini. Ajali za mara kwa mara nchini humo katika eneo la migodi ni jambo la kawaida.