Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 14:32

Wachambuzi wataka suluhisho la haraka Zanzibar


Raia akitumia haki yake ya kupiga kura,October 25, 2015.
Raia akitumia haki yake ya kupiga kura,October 25, 2015.

Nchini Tanzania baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa walizungumzia mzozo wa kisiasa unaoendelea visiwani Zanzibar baada ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar-ZEC kufuta uchaguzi mkuu visiwani humo uliofanyika oktoba 25 mwaka huu.

Huku kukiwa na taarifa kadhaa juu ya juhudi za kuupatia ufumbuzi mgogoro huo mpya wa kiasaisa Zanzibar ikiwemo mazungumzo baina ya viongozi wa juu na wakuu wa vyombo vya usalama, wachambuzi mbalimbali wa masuala ya kisiasa nchini walikuwa na maoni tofauti juu ya suluhisho la mzozo huo kwa sasa ambapo chama cha wananchi CUF kupitia mgombea wake visiwani humo Maalim Seif Shariff Hamad, kikidai kuwepo mizengwe ya makusudi kuwanyima ushindi.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:40 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


Dr. Benson Bana mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar Es Salaam katika mahojiano maalum Jumatatu jijini Dar Es Salaam alitaka kuwepo kwa maridhiano ya kisiasa kama ilivyokuwa wakati wa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa visiwani humo uliomaliza mgogoro wa kisiasa wa muda mrefu.


Akizungumzia tetesi kwamba kuna wasuluhishi kutoka nje ya Tanzania wamewasili Zanzibar kushughulikia mzozo huo, Dr. Bana alisema kwa upande wake anaamini viongozi wa ndani ya Tanznaia wana uwezo wa kusuluhisha mgogoro huo wa kisiasa.


Wakati huo huo chama cha upinzania cha ADC nacho kiliitaka serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, pamoja na vyama vya CUF na CCM kutafuta muafaka kwa njia ya mazungumzo kuhusiana na suala la kufutwa kwa uchaguzi huo wa Octoba 25 kama njia ambayo itaepusha Zanzibar kutumbukia katika machafuko.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar-ZEC, bwana Jecha Salim Jecha alitangaza kufuta uchaguzi wa Zanzibar kwa madai ya kuwepo kasoro nyingi katika zoezi hilo.

XS
SM
MD
LG