Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 03:57

Wabunge waliotimuliwa na Chadema kusalia bungeni licha ya tetesi za chama


Aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Chadema Tundu Lissu akipiga kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Lisu amekosoa uamuzi wa spika kuhusu wabunge maalum wa chama chake
Aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Chadema Tundu Lissu akipiga kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Lisu amekosoa uamuzi wa spika kuhusu wabunge maalum wa chama chake

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, cha demkorasia na maendeleo – CHADEMA, kimesisitiza kwamba waliokuwa wabunge wake, waliotimulia na chama, wanastahili kuvuliwa ubunge licha ya mahakama kuu kuamua kwamba watanedelea kuhudumu hadi uamuzi kamili wa mahakama utakapotolewa.

Mahakama kuu iliamua kwamba wabunge hao maalum 19 wataendelea kushikilia nafasi zao bungeni hadi uamuzi wa kesi walioasilisha mahakamani kupinga kufurushwa kwao na chama, itakapoamuliwa.

Naibu wa chama cha Chadema Tundu Lisu, amemshutumu spika wa bunge Dr. Tulia Ackson, akisema kwamba uamuzi kuhusu wabunge hao maalum 19 umechochewa kisiasa.

Dr. Ackson amesema kwamba hahusiki kwa namna yotote na kesi hiyo na kwamba alichukua uamuzi wake wa kuagiza wabunge hao kuendelea kuwa bungeni baada ya kugundua kwamba kesi yao ilikuwa bado mahakamani jijini Dar es Salaam.

Ackson amesisitiza kwamba “Bunge haliwezi kuingilia kesi ambayo ipo mahakamani. Tutasubiri mahakama ifanye uamuzi wake ndipo tuchukue hatua.”

Lakini Tundu Lissu amedai kwamba mbunge anapopoteza kiti chake bungeni kwa sababu yoyote ile, anastahili kuondolewa bungeni mara moja.


“Wanstahili kuwa nje ya bunge hadi mahakama kuu itakapofanya uamuzi wake,” amesema Lissu akiongezea kwamba “hivyo ndivyo ilivyokuwa dhidi yangu nilipofurushwa na aliyekuwa spika Job Ndugai.”

Lissu amesema kwamba alienda mahakamani kujaribu kubatilisha uamuzi wa spika lakini kesi yake ilikataliwa. Rufaa yake haikusikilizwa hadi bunge la 11 lilipovunjwa.

Uamuzi kama huo ulichukuliwa dhidi ya aliyekuwa mbunge Godbless Lema, sawa na wabunge 8 wa chama cha CUF, walipofukuzwa na chama chao mwaka 2017 waliofurushwa bungeni japo waliasilisha kesi mahakamani.


Mkuu wa mawasiliano wa Chadema John Mrema, amesema kwamba “alichosema Tundu Lisu ndio msimamo wa chama na kwamba msimamo wa Spika ni wa kisiasa.”

Wabunge maalum 19 wa Chadema, walifukuzwa rasmi wiki iliyopita kutoka kwa chama baada ya baraza kuu la chama hicho kufanya uamuzi wa mwisho, lakini Spika Ackson amesema kwamba wakati alipokea taarifa ya chama cha Chadema, wabunge hao tayari walikuwa washawasilisha kesi katika mahakama kuu kupinga kufurushwa kwao.


“Kulingana na katiba yetu, mahakama ndio yenye jukumu la kuhakikisha kwamba kuna haki. Kwa hivyo, katika nchi inayoheshimu sheria, idhara nyingine haiwezi kuingilia kazi ya nyingine,” amesema spika Ackson akiongea kwamba “kama mtu yeyote ana swali, basi akaulize mahakama, na Mahakama itakapochukua uamuzi wake, nitakuja hapa na kutangaza msimamo wa bunge.”

Wabunge hao 19 walikuwa wamepoteza nafasi zao katika uchaguzi wa mwaka 2020 lakini waliapishwa kama wabunge maalum, hatua ambayo ilikasirisha uongozi wa chama chao kilichokuwa kikipinga matokeo ya uchaguzi huo kikisema kwamba ulikuwa na dosari, na kupinga ushindi wa aliyekuwa rais John Magufuli na chama kinachotawala cha CCM.

XS
SM
MD
LG