Wabunge wa Marekani wamerejea katika kikao wiki hii baada ya mapumziko ya wiki tatu ya kipindi cha sikukuu, ili kuendelea na kazi kuelekea makubaliano kuhusu usalama wa mpaka kwa mabadilishano ya kupata kura za Warepublican, ili waweze kupeleka misaada zaidi kwa Ukraine.
“Tunakaribia kufikia makubaliano kuliko tulivyokuwa tangu kuanza kwa mazungumzo haya”, Seneta wa chama cha Democratic Chris Murphy, mmoja wa wajumbe wakuu wa mazungumzo juu ya makubaliano hayo, aliwaambia waandishi wa habari Jumanne.
“Natamani tusingekuwa katika nafasi hii. Ninatamani kwamba Wa-republican katika Seneti waunge mkono msaada wa Ukraine kwa sababu wanaiamini Ukraine”, alisema. “Natamani kwamba tusingekuwa na masharti ya misaada kwa Ukraine juu ya azimio la suala gumu zaidi katika siasa za Marekani, mageuzi ya uhamiaji.
Ombi la ziada la usalama wa taifa la White House la dola bilioni 106 pia linajumuisha ufadhili wa usalama wa mpakani, pamoja na karibu dola bilioni 14 za msaada kwa Israel na ufadhili kwa Taiwan kupambana na kitisho kinacholetwa na China.
Forum