Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 11:41

Wabunge wa Marekani walaumiana kutokana na kufungwa kwa serikali


Wabunge wa Republikan wakitoa shutuma zao.
Wabunge wa Republikan wakitoa shutuma zao.
Wamarekani wameanza kuingiwa na wasi wasi na kuuliza lini mvutano wa kisiasa utakapomalizika bungeni. Hii yote inatokana na kwamba siku ya jumanne siku ya pili ya tangu kusita kwa sehemu kubwa ya kazi za serikali wabunge walikuwa wakikashifiana.

Warepublikan walipendekeza mipango midogo midogo ya kutoa ili kugharmia kufungua baadhi ya maeneo maarufu yanayoendeshwa na serikali. Seneta Ted Cruz amehimiza kutolewa fedha za dharura kwa ajili ya maeneo ya hifadhi za taifa na idara ya wanajeshi wa marekani waliostahafu.

Kiongozi wa walio wengi kwenye baraza la seneti Harry Reid amesema wazo hilo haliingi akilini. Seneta mwenzake wa chama cha Democratic Richard Durbin aliieleza hiyo kuwa ni tusi kabisa.

Hadi kufikia mwisho wa siku utoaji mipango ya kutoa fedha kidogo kidogo haukufanikiwa. Lakini kitendo hicho kilipelekea wademokrat katika nafasi wasiyopenda ya kupinga kufungua sehemu ndogo ya shughuli za serikali na hivyo kusaidia juhudi za warepublikan kujionyesha kuwa wao ni watu wanaotaka kupatikana ridhaa ya maana na wademokrat kuonekana kuwa wabishi.

Juhudi hizo zilianza mapema katika siku hiyo wakati baraza lililoongozwa na warepublikan lilipopiga kura kutaka kuanza mazungumzo na baraza la senet juu ya kufungwa kwa shughuli za serikali. Mbunge Mrepublikan Tom McClintock amesema hivyo ndivyo Baraza la Wawakilishi linavyotakiwa kufanya kazi.

Mvutano huo wote unatokana na sheria ya huduma za afya ya Rais Barack Obama, sehemu kubwa ambayo imeanza rasmi jumanne.Warepublikan wametaka kuondoa fedha au kuchelewesha utekelezaji wa sheria na warepublikan wengi wamekataa kupiga kura kuidhinisha bajeti ya matumizi bila ya kuwepo na vipengele vya kuharibu sheria hiyo ijulikanayo Obama care.

Maseneta Wademokrat wanasema wako tayari kufanya mazumgumzo ya pande mbili lakini si wakati serikali imefungwa. Kiongozi wa walio wengi Harry Reid, alitowa wito kwa wabunge kupitisha muswaada wa bajeti usio na masharti yeyote ya kisiasa.

Uchunguzi wa awali wa maoni unaonyesha wengi wa wananchi wa Marekani wanawashutumu Warepublikan kuliko Wademokrat na Rais Obama kwa kufungwa kwa serikali.
XS
SM
MD
LG