Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 14:34

Wabunge wa Kenya wakemea mauaji holela yaliyofanyika nchini humo


Wabunge ndani ya kikao cha bunge wakizungumzia mauaji holela yaliotokea katika maeneo kadhaa ya Kenya
Wabunge ndani ya kikao cha bunge wakizungumzia mauaji holela yaliotokea katika maeneo kadhaa ya Kenya

Wabunge nchini Kenya, Jumatano walikuwa na mjadala maalumu juu ya kukabiliana na vitendo vya mauaji holela yaliyofanyika kwenye maeneo mbali mbali ikiwemo Mandera, Pwani na Kapedo.

Wabunge hao walilaani vikali mauaji na visa vinavyohusiana na harakati za kigaidi zinazohusisha vijana ambao inasemekana wanajihusisha na vitendo vya uhalifu kutokana na ukosefu wa ajira na viongozi wa kaunti kutowawezesha wakazi wa maeneo yao ikiwemo utoaji elimu ya umma kwa vijana nchini humo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:05:00 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Sauti ya Amerika-VOA ilizungumza na mbunge Thomas Mwadegu wa Kaunti ya Taita-Taveta ambaye anaanza kwa kuelezea hatua zinazofanywa na serikali hivi sasa kusitisha mauaji holela kwa wananchi.

Miongoni mwa matukio yanayoshukiwa ya kigaidi
Miongoni mwa matukio yanayoshukiwa ya kigaidi

Wakati huo huo polisi huko Mombasa ilisema zaidi ya vijana 200 tayari wameachiwa huru bila kufunguliwa mashtaka yeyote kuhusiana na operesheni ya kuwasaka wahusika wa mafunzo ya itikadi kali za kidini.

Hayo yalisemwa Jumatano katika mahakama ya Mombasa ambako watu 24 waliokuwa miongoni mwa watu 251 waliokamatwa wameshtakiwa rasmi na polisi lakini misikiti mine bado imeendelea kufungwa.

XS
SM
MD
LG