Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 21:59

Wabunge wa Israel wapitisha sheria ya kumrejesha Ntenyahu mamlakani


Benjamin Netanyahu muda mfupi baada ya kushinda kwenye uchaguzi wa Novemba. Nov 2, 2022.
Benjamin Netanyahu muda mfupi baada ya kushinda kwenye uchaguzi wa Novemba. Nov 2, 2022.

Bunge la Israel Jumanne limepitisha sheria yenye  utata itakayomrejesha mwanasiasa wa siku nyingi Benjamin Netanyahu kwenye wadhifa wa waziri mkuu.

Kufuatia ushindi wake katika uchaguzi wa Novemba mosi, Netanyahu alipata mamlaka ya kuunda serikali inayoungwa mkono na vyama vya Othodox vya kiyahudi pamoja na vile vya mrengo wa kulia. Wachambuzi wanasema kwamba Netanyahu Alhamisi atawasilisha bungeni serikali yenye msimamo mkali zaidi wa kulia kwenye historia ya Israel.

Sheria hiyo mpya inamruhusu mtu yeyote aliyepatikana na hatia bila kupewa adhabu ya kifungo awe na nafasi ya kuhudumu kama mawaziri. Kabla ya sheria hiyo kupitishwa, kulikuwa na hali ya kutokuwa na uhakika iwapo Aryeh Deli ambaye ni mshirika mkuu chama cha ki Orthodox cha Shas angeweza kuhudumu serikalini kutokana na kushtakiwa awali kwa kukwepa kulipa kodi.

Sheria ya pili iliyopitishwa pia inawaruhusu mawaziri wawili kuhudumu kwenye ofisi moja.

XS
SM
MD
LG