Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 19:31

Wabunge wa Gambia wapitisha kuendelea marufuku ya ukeketaji


Wabunge wa Gambia Jumatatu wamepitisha mapendekezo ya kuendeleaza marufuku yake ya ukeketaji kabla ya kura itakayopigwa baadaye mwezi huu ya kama itaharamisha mila hiyo.

Ukeketaji umepigwa marufuku Gambia toka mwaka 2015, lakini mila hiyo iliyokita mizizi bado imeenea katika taifa hilo la Afrika Magharibi na hukumu za kwanza mwaka jana zilichochea upinzani dhidi ya sheria hiyo.

Baada ya mjadala mkali Jumatatu, mapendekezo yaliyomo katika ripoti ya kamati ya pamoja ya afya na jinsia yaliidhinishwa na kikao cha bunge, huku wabunge 35 wakipiga kura ya kuunga mkono kupitishwa kwa ripoti hiyo, 17 wakipinga na wawili hawakuhudhuria.

Kura ya mwisho kuhusu mswada wa kuharamisha ukeketaji kwa sasa imepangwa kufanyika Julai 24.

Iwapo bunge litaiidhinisha, Gambia itakuwa nchi ya kwanza kubatilisha marufuku ya ukeketaji.

Ilipitisha usomaji wake wa pili mwezi Machi na wabunge watano tu kati ya 53 walipiga kura dhidi yake na mmoja kutoshiriki.

Forum

XS
SM
MD
LG