Wabunge wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameteua tume maalum kutayarisha mswada wa kubadili kifungu cha katiba kufutilia mbali duru ya pili ya uchaguzi.
Wabunge wa upinzani wamesusia vikao vya kubadilisha kifungu hicho cha katiba wakisema inakwenda kinyume na demokrasia na ni hatua ya kukandamiza upinzani.
Wabunge wa chama tawala watajadili mabadiliko hayo Jumamosi kabla ya kufunga bunge kwa msimu huu.