Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 17:59

Waasi wavamia makazi ya Gadhafi mjini Tripoli


Wapiganaji waasi wakionyesha ishara ya ushindi katika wilaya ya Gorgi mjini Tripoli.
Wapiganaji waasi wakionyesha ishara ya ushindi katika wilaya ya Gorgi mjini Tripoli.

Milio ya bunduki na milipuko inaendelea kusikika katika mji mkuu wa Libya.

Mamia ya waasi wamevamia makazi ya kiongozi wa Libya, Moammar Gadhafi katika mji mkuu Tripoli, wakati viongozi wa waasi wanasema wanadhibiti sehemu nyingi za mji huo.

Wapiganaji waasi walipigana hadi kuingia katika makazi ya bwana Gadhafi ya Bab al-Aziziya huku wakikumbana na mashambulizi makali ya wanajeshi wanaoumuunga mkono Gadhafi. Dazeni ya waasi walionekana wakipiga risasi hewani kusherehekea kile kinachoelezewa ushindi mkubwa.

Moshi mweusi ulitanda angani wakati milio ya bunduki na milipuko iliendelea kusikika kuzunguka makazi hayo na sehemu kadhaa za mjini humo.

Waziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton amesema kiongozi wa kisiasa wa upande wa waasi, Mustafa Abdel Jalil alimueleza kuwa wanadhibiti asilimia 80 ya mji mkuu wa Libya.

Msemaji wa NATO, Oana Lungescu, aliwaambia waandishi wa habari mjini Brussels kwamba operesheni ya NATO nchini Libya haijakwisha, na kwamba wataendelea na operesheni za kijeshi mpaka mashambulizi yote na vitisho vya mashambulizi dhidi ya rais vimalizike kabisa.

Msemaji wa NATO Kanali Roland Lavoie aliongezea kwamba majeshi ya NATO hayamlengi kabisa bwana Gadhafi, lakini ushirika huo utashambulia pale ambapo inaona kuna umuhimu nchini Libya ili kuwalinda raia.

Bwana Gadhafi hajulikani mahali alipo. Lakini mtoto wake wa kiume na ambaye alitarajiwa angekuwa mrithi wake, Seif al-Islam, alijitokeza mjini humo Jumatatu usiku akisema baba yake bado yuko Tripoli na kwamba serikali yake bado ina udhibiti.

XS
SM
MD
LG