Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 11:50

Waasi wampa Assad saa kadhaa za kusitisha mapigano


Mwakilishi wa amani wa kimataifa Kofi Annan( kati kushoto), Rais wa Syria Bashar al-Assad (kati kulia) pamoja na wawakilishi wengine wa kimataifa juu ya Syria
Mwakilishi wa amani wa kimataifa Kofi Annan( kati kushoto), Rais wa Syria Bashar al-Assad (kati kulia) pamoja na wawakilishi wengine wa kimataifa juu ya Syria

Hatua hiyo imefuata baada ya serikali ya Assad kushindwa kutekeleza mwongozo uliotolewa na bwana Annan mwezi uliopita

Kamanda mmoja wa waasi nchini Syria anasema majeshi yake yatatupilia mbali mkataba wa kusitisha mapigano na serikali siku ya Ijumaa kama Rais Bashar al-Assad anashindwa kufuata mwongozo wa makubaliano na vipengele vingine vya mpango wa amani unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Katika taarifa iliyosambazwa kwenye internet Alhamis, Kanali Qassim Saadeddine wa kundi la Free Syrian Army-FSA alimpa bwana Assad muda hadi Ijumaa mchana kwa saa za Syria kuanza kutekeleza mwongozo uliotolewa na mwakilishi wa amani wa kimataifa Kofi Annan. Kamanda huyo wa waasi alisema majeshi yake hayatafuata tena mpango wa amani uliowekwa na bwana Annan kama Rais wa Syria anashindwa kutekeleza hilo.

FSA ni kundi la uasi lililo na silaha ambalo linajumuisha wanajeshi waasi. Limekuwa likiongoza kwa muda wa miezi 15 katika vuguvugu za kuumaliza utawala wa miaka 11 wa bwana Assad. Serikali ya Syria na waasi walikubaliana kusitisha mapigano kwenye mazungumzo na mpatanishi wa amani bwana Annan mwezi uliopita, lakini mapigano bado yanaendelea na kila upande unamshutumu mwenzie kwa kukiuka makubaliano hayo.

Wanaharakati wa haki za binadamu nchini Syria walisema majeshi ya serikali yalifyatua makombora na risasi kwenye mji wa kati wa Houla hapo Alhamis na kumuuwa mtu mmoja takribani wiki moja baada ya raia 108 kuuwawa katika eneo hilo kufuatia shambulizi ambalo lilizusha wasiwasi wa kimataifa.

XS
SM
MD
LG