Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 14:20

Waasi wameteka miji mikubwa miwili nchini DRC


Waasi wa M23 wakitembea katika mji wa Karuba uliopo kilomita 62 magharibi ya Goma huko mashariki mwa DRC. (Picha hii imechukuliwa kutoka matukio yaliyopita)
Waasi wa M23 wakitembea katika mji wa Karuba uliopo kilomita 62 magharibi ya Goma huko mashariki mwa DRC. (Picha hii imechukuliwa kutoka matukio yaliyopita)

Mapigano kati ya jeshi la Kongo na waasi wa M23 yaliongezeka karibu na ujirani  wa Rutshuru na Kiwanja siku ya Jumamosi, huku milio ya risasi ikizuka  wakati wa asubuhi

Waasi wameteka miji miwili mikubwa mashariki mwa Kongo baada ya mapigano makali siku ya Jumamosi, na kuongeza maradufu eneo wanalolidhibiti sasa, kiongozi wa mashirika ya kiraia na wakaazi wamesema.

Mapigano kati ya jeshi la Kongo na waasi wa M23 yaliongezeka karibu na ujirani wa Rutshuru na Kiwanja siku ya Jumamosi, huku milio ya risasi ikizuka wakati wa asubuhi.

John Banyene, rais wa mashirika ya kiraia nchini humo, aliliambia shirika la habari la Associated Press kwamba waasi sasa wanadhibiti kituo cha Rutshuru na Kiwanja, maeneo hayo yako kilomita 70 kutoka mji mkuu wa jimbo, Goma.

Wakati tunapozungumza, tunathibitisha kwamba waasi wa M23 na washirika wao wanadhibiti mji wa Kiwanja, lakini vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo havijakata tamaa," Banyene aliwaambia waandishi wa habari mjini Goma.

Hakuna uthibitisho wa haraka kutoka kwa mamlaka ya Kongo au jeshi juu ya kukamatwa kwa miji hiyo miwili.

Daniel Subuka, mkazi wa Kiwanja aliyewasiliana kwa njia ya simu na shirika la habari la AP, alisema aliwaona waasi wa M23 waliokuwa wamejhami vizuri kwa silaha wakiingia Kiwanja na wengine wakielekea kituo cha Rutshuru.

Waasi wa M23 kwa kiasi kikubwa hawakuwa wakifanya harakati zozote kwa takriban muongo mmoja kabla ya kuibuka tena Novemba mwaka jana huko mashariki mwa Kongo. Mamlaka zinasema karibu watu 200,000 wameyakimbia makazi yao hata kabla ya ongezeko la hivi karibuni la ghasia katika kipindi cha wiki moja iliyopita.

XS
SM
MD
LG