Viongozi wa DRC, Burundi, Rwanda na rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye ni mpatanishi katika mzozo huo, walikutana mjini Luanda, Angola, katika mkutano ulioandaliwa na rais wa Angola.
Mkutano wa Luanda uliamua kwamba iwapo M23 hawatatii agizo hilo la kuweka silaha chini leo Ijumaa na kuondoka kwenye ngome mpya, majeshi ya kikanda yaliyopelekwa mashariki mwa DRC yatatekeleza agizo hilo.
Kundi la M23 hivi sasa linadhibiti sehemu kubwa ya jimbo la Kivu Kaskazini na linatishia kuuteka mji wa Goma, mji mkuu mashariki mwa Congo.