Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 21:06

Waasi wa M23 'waangusha' ndege ya UN


Ndege ya Umoja wa mataifa ikipaa juu ya mbuga ya wanyama ya kitaifa ya Virunga July 11, 2012. Picha ya AFP
Ndege ya Umoja wa mataifa ikipaa juu ya mbuga ya wanyama ya kitaifa ya Virunga July 11, 2012. Picha ya AFP

Waasi wa M23 wamekanusha ripoti kwamba walitengua ndege ya wanajeshi wa kulinda amani wa umoja wa mataifa, na kusababisha vifo vya wanajeshi wanane, mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Jeshi la Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wamedai kwamba waasi wa M23 ndio walitengua ndege hiyo na kusababisha vifo vya wanajeshi sita wa Pakistan, mmoja wa Russia na mwingine wa Serbia.

Ndege hiyo ilianguka katika mkowa wa Kivu kaskazini, ambapo mapigano makali yamekuwa yakiendelea kati ya waashi wa M23 na wanajeshi wa DRC.

Waasi wa M23, ambao walikuwa wamekimbia kutoka DRC mwaka 2013, wamejikusanya na kuchukua udhibithi wa sehemu muhimu nchini DRC tangu jumatatu.

Umoja wa mataifa umesema kwamba zaidi ya watu 13,000 wamekimbia makwao na wengi wako kuingia Uganda kama wakimbizi kutokana na mapigano makali kati ya waasi hao wa M23 na wanajeshi wa serikali.

XS
SM
MD
LG