Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 08:57

Waasi wa Libya wameitwaa tena miji kadhaa ya ufukweni


Waasi wa Libya karibu na Ras Lanouf. (AP Photo/Anja Niedringhaus)
Waasi wa Libya karibu na Ras Lanouf. (AP Photo/Anja Niedringhaus)

Majeshi ya waasi wa Libya yamefanikiwa kusonga mbele kwa haraka, wakichukua tena bandari muhimu za miji ya mafuta

Waasi wa Libya wameitwaa tena miji kadhaa ya ufukweni inayokaribiana na Sirte, baada ya mashambulizi ya makombora kutoka ndege za majeshi ya muungano wa NATO .

Mwandishi wa VOA Edward Yeranian anaripoti kuwa majeshi ya waasi wa Libya yamefanikiwa kusonga mbele kwa haraka, wakichukua tena bandari muhimu za miji ya mafuta za Ras Lanouf na Brega, ambazo zilitwaliwa na majeshi ya serikali takribani siku kumi zilizopita.

Mashahidi wanasema majeshi ya serikali yalijitoa katika eneo hilo bila mapigano yoyote. Baadhi ya wanajeshi waliobaki eneo hilo walijisalimisha.

Televisheni ya Al-Arabia Jumapili ilionyesha picha za vifaru vya serikali vilivyoteketezwa pamoja na magari ya kijeshi katika barabara kuu ya pwani inayoelekea mji wa Ras Lanouf. Pia ilionyesha video ya ndege za Uingereza zikilipua maeneo kadhaa yanayokaliwa na Gadhafi.

Wanajeshi waasi wameiambia Televisheni ya Al-Jazeera kwamba harakati zao zijazo zitaelekezwa mji wa bandari ya Sirte, mji anaotoka kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi. Kanali wa zamani wa jeshi ambaye amejiunga na waasi amesema kuwa majeshi yanayomtii Gadhafi yametega mabomu ya ardhini kuzunguka mji wa Sirte.

watamwacha kadri shinikizo la kijeshi linavyozidi kumkabili.

XS
SM
MD
LG