Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 05:42

Waasi wa kundi la M23 wamtimua kiongozi wao


Askofu Jean Marie Runiga
Askofu Jean Marie Runiga

Jean Marie Runiga atimuliwa kama kiongozi wa M23.Kiongozi mpya ni Sultan Makenga

Kundi la waasi la M23 la nchini DRC limemfukuza kiongozi wake Jean-Marie Runiga likimshutumu kwa makosa ya uhaini na matumizi mabaya ya fedha.

Kundi hilo lilitoa taarifa ikisema Runiga alimruhusu Bosco Ntaganda, jenerali wa zamani wa Congo kushawishi maamuzi ya kundi hilo kwa kiwango kikubwa na kuchochea ghasia miongoni mwa waasi.

Wanasema Runiga pia alishindwa kutekeleza malengo ya kisiasa ya kundi hilo. Msemaji wa kundi la M23, Bertrand Bisimwa alithibitisha mabadiliko hayo ya uongozi kwa Sauti ya Amerika-VOA na kusema Runiga huenda amekimbia kuungana na Ntaganda.

Watu wasiopungua wanane walikufa katika mapigano Jumapili jioni kati ya wapiganaji watiifu wa mkuu wa jeshi la M23, jenerali Sultani Makenga na wafuasi wa kiongozi mwingine. Waasi wamemteuwa Sultan Makenga kuwa mkuu wao mpya wa muda.
XS
SM
MD
LG