Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 19:02

Waasi Libya wachukua udhibiti wa miji miwili kusini mwa Tripoli

mpiganaji muasi akionesha ishara ya ushindi baada ya mapigano ya kugombea mji wa Al-Qawalish Julai 6, 2011.
mpiganaji muasi akionesha ishara ya ushindi baada ya mapigano ya kugombea mji wa Al-Qawalish Julai 6, 2011.

Majeshi ya waasi yamesema jumatano yamechukua udhibiti wa mji wa Al- qawalish na Kikla yote ikiwa kilomita 100 kutoka mji wa Tripoli ulio ngome ya bwana Gadhafi.

Waasi wa libya wamechukua udhibiti wa miji miwili midogo kusini mwa Tripoli katika mashambulizi ya masaa sita na majeshi yanayomtii kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi wakati wapiganji wa upinzani mashariki mwa mji mkuu wakishindwa vikali katika mapigano na serikali.

Majeshi ya waasi yamesema jumatano yamechukua udhibiti wa mji wa Al- qawalish na Kikla yote ikiwa kilomita 100 kutoka mji wa Tripoli ulio ngome ya bwana Gadhafi.

Mji unaofuatia kwa ukubwa kaskazini ni Garyan ambao unadhibiti barabara kuu inayoelekea kwenye mji mkuu.

Wapiganaji wa upinzani pia walisogea ndani zaidi kutoka kwenye ngome yao ya Misrata kuelekea mji wa Zlitan lakini Walishambuliwa vikali.

Wafanyakazi wa huduma za afya wanasema takriban waasi 14 waliuwawa na wengine 30 walijeruhiwa katika mapigano karibu na mji jumatano.

XS
SM
MD
LG