Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 27, 2024 Local time: 02:58

Waandishi habari wakusanyika mbele ya ofisi za Daily Monitor


Tishio kwa wapenzi wa jinsia moja lilitoka kwenye gazeti la Daily Monitor
Tishio kwa wapenzi wa jinsia moja lilitoka kwenye gazeti la Daily Monitor
Kwa siku ya kumi sasa magazeti ya The Daily Monitor na Redpepper pamoja na radio za K-fm na Dembe fm zingali zimefungwa. Waandishi habari kutoka vyombo tofauti vya habari kwa siku ya pili wamekuwa wakifanya maandamano ya amani mbele ya ofisi za The Daily Monitor kama njia ya kuonyesha mshikamano na waandishi wa magazeti yaliyofungwa.

Polisi imekuwa ikiitafuta barua iliyoandikwa na mkuu wa vitengo vya ujasusi Jenerali David Sejusa Tinyefuza akidai kuwa baadhi ya maafisa wakuu serikalini wana mpango wa kuwauwa maafisa wengine wakuu wa serikali na jeshi ambao wanapinga mpango wa rais Yoweri Museveni akishirikiana na maafisa wa juu wa usalama nchini Uganda wa kuhakikisha kuwa mwana wa rais Museveni, Brigedia Muhoozi .

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:00 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Kaneirugaba anateuliwa kuwa rais wakati baba yake atakapong'atuka mamlakani.
Ni sauti za waandishi habari wakibishana na askari polisi aliyekuwa anawaamrisha waondoke walipokuwa wamesimama takriban mita hamsini kutoka kwenye ofisi za gazeti la The Daily Monitor la sivyo, polisi ingetumia nguvu kuwaondoa pale.

Waandishi habari walipokataa kuondoka Polisi wakafyatua risasi na kisha kuwatupia waandishi habari gesi ya kutoa machozi. Walitawanyika kwa muda na kukusanyika tena. Wakawasogelea askari polisi bila uwoga. Yaliyotoka vinywani mwa baadhi ya waandishi habari?

Litakuwa jambo la kushangaza ikiwa utamuumiza mmoja wetu kwa sababu ya amri za kijinga. “Sisi ni waandishi habari na tumekuwa tukipigania haki zenu. Angalieni mnapolala, wake zenu juzi walikuwa wanaandamana kwa sababu ya maisha duni wanayoishi na wengi wenu mna njaa kwa sababu kwa kipindi cha siku kadhaa zilizopita hamjakuwa mkipata chakula.


Mna haki ya kufanya kazi kama polisi na sisi kama waandishi habari pia tuna haki ya kufanya kazi na wanapigania haki yao ya kufanya kazi. Hatupigani na nyinyi. Tinyefuza aliyeandika barua mnayoitafuta yuko Uingereza. Kwa nini msiende huko mkammate? Kwa nini mwakamate waandishi wanaofanya kazi yao. Wake zenu wameandamana kupinga kukandamizwa kwa waume zao na mnawazuia waandishi habari wasiandamane? Ni jambo la kufurahisha.

Sisi ndio tunaandika ripoti kuhusu jinsi mnavyoishi na vile pesa zenu zinavyoliwa na sasa mnatitupia gesi ya kutoa machozi. Kitendo chenu kina maana yoyote kwenu?”
Waandishi habari wameapa kuwa watakuwa wanakwenda kwenye ofisi za the Daily Monitor kila siku na kufanya maandamano hadi gazeti hili litakapofunguliwa tena.

Shirika la kutetea haki za waandishi habari Alhamisi litakwenda mahakamani kumshtaki mkuu wa polisi, mkuu wa sheria, taasisi ya mawasiliano pamoja na jeshi kwa kuzifunga ofisi za The Daily monitor na Redpepper pamoja na radio za Kfm na Dembe FM.

Wakati huo huo waandishi habari wa Redpepper nao wanasema maisha yamekuwa magumu na hawajui la kufanya kwa sababu baadhi ya watoto wao hawakurudi shuleni jumatatu ya wiki hii baada ya shule kufunguliwa kwa muhula wa pili. Sasa wanasema watatafuta njia nyingine za kujikimu kimaisha. Haijulikani vyombo vya habari vilivyofungwa vitafunguliwa lini.
XS
SM
MD
LG