Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 25, 2025 Local time: 08:10

Waandishi wa habari wawili Sudan Kusini wameachiwa huru


Baadhi ya magazeti yanayochapishwa Sudan Kusini
Baadhi ya magazeti yanayochapishwa Sudan Kusini

Kundi linaloangazia vyombo vya habari lilisema Jumatano wakati lilipodai kutolewa kwa wenzao wawili. Waandishi wawili kati ya saba waliokamatwa Januari bado wanashikiliwa kwenye kizuizi cha polisi kufuatia video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii mwezi Disemba UJOSS kilisema

Waandishi wa habari wawili wa Sudan Kusini waliokamatwa kufuatia kusambaa kwa video iliyomuonyesha rais Salva kiir akijisaidia haja ndogo, wameachiwa huru.

Kundi linaloangazia vyombo vya habari lilisema jumatano wakati lilipodai kutolewa kwa wenzao wawili. Waandishi wawili kati ya saba waliokamatwa January bado wanashikiliwa kwenye kizuizi cha polisi kufuatia video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii mwezi Disemba chama cha waandishi wa habari Sudan Kusini (UJOSS) kilisema.

Waandishi wa habari, wafanyakazi kwenye chombo cha habari cha serikali walikamatwa na wakala kutoka kitengo cha usalama wa taifa Sudan kusini kama sehemu ya uchunguzi kuhusiana na chanzo cha video hiyo.

Katika picha ya video, Kiir ambaye alikuwa amevalia nguo za kahawia na kofia nyeusi alionekana suruali yake kuloa kwenye mguu wa kushoto.

XS
SM
MD
LG