Mahamaka nchini Zimbabwe imetoa dhamana kwa waandishi watatu wa habari waliokamatwa kwa kuchapisha taarifa iliyohusisha maafisa wa polisi kwenye kadhia ya uwindaji haramu wa tembo.
Licha ya kuwepo mjadala wa saa tatu kutoka kwa waendesha mashtaka wa serikali, Tendai Mahwe alitoa amri Jumatano kuwa waandishi wote watatu waachiliwe kwa dhamana ya dola 100.
Foster Dongozi kutoka jumuiya ya waandishi wa habari amesema watatu hao hawakustahili kukamatwa. Waandishi hao kutoka gazeti la The Sunday Mail, walikamatwa jumatatu karibu kilomita 700 kusini magharibi mwa Harare.