Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 10:52

Waandishi wa habari Uganda walalamikia kukamatwa


Polisi wa Uganda wawazuilia wanahabari wa gazeti la Daily Monitor kuondoka afisini zao mjini Kampala kwa tuhuma kwamba gazeti hilo liliandika tahariri ya kuikashfu serikali.
Polisi wa Uganda wawazuilia wanahabari wa gazeti la Daily Monitor kuondoka afisini zao mjini Kampala kwa tuhuma kwamba gazeti hilo liliandika tahariri ya kuikashfu serikali.

Chama cha waandishi wa habari nchini Uganda kimeeleza hofu kuhusu jinsi wanahabari wanavyoendelea kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uhaini.

Hii Hayo yalijiri baada ya waandishi wa habari watatu kukamatwa katika mazingira ya utatanishi na kushutumiwa kwa njama ya kujaribu kuipindua serikali, mashtaka ambayo adhbu yake ni kifo wakikutwa na hatia.

Ripoti za waandishi wa habari kutekwa nyara na watu wasiojulikana nchini Uganda na kisha baadaye kupatikana gerezani baada ya siku kadhaa zimekera muungano wa waandishi na kuzua hofu kubwa miongoni mwao.

Jumatatu asubuhi, mwandishi wa kituo cha habari cha kibinafsi chaTop Radio Richard Kasule alitekwa nyara nje ya ofisi za kituo hicho muda mfupi baada ya kuandaa matangazo ya asubuhi.

Wenzake katika kituo hicho cha habari walidai kwamba Kasule alikamatwa na polisi baada ya kufichua ushirikiano kati ya walinda usalama na makundi ya uhalifu jijini Kampala.

Mtangazaji huyo aliandaa kipindi cha saa nzima akiwahoji viongozi wa makundi hayo ya uhalifu waliodai kushirikiana na polisi bila kukamatwa.

Hatua ya kukamatwa kwa kasule inajiri siku mbili baada ya mwandishi wa gazeti la serikali la the new vision, Charles Etukuri, kukamatwa nje ya ofisi za gazeti hilo la serikali.

Etukuri alichapisha taarifa ya upekuzi kuhusiana kifo cha mwekezaji kutoka bara ulaya katika hoteli moja maarufu jijini Kampala, na kukamatwa kwa viongozi wakuu 6 wa polisi kisiri.

Mwandishi mwingine wa habari Isaac Bakka, aligunduliwa akiwa amezuiliwa katika gereza la Luzira nje kidogo ya jiji la Kampala, baada ya kutoweka katika mazingira ya kutatanisha.

Msemaji wa mahakama Solomon Muyita, aliiambia sauti ya Amerika Jumatatu kwamba mwandishi huyo alikuwa ameshafunguliwa mashtaka ya uagizaji wa silaha hatari kwa nia ya kuipindua serikali yake Yoweri Museveni.

Wahairi wa gazeti la upekuzi la red pepper, radio ya juice FM na gazeti linalochapishwa kwa lugha ya kiganda la 'Kamunye,' nao wanakabiliwa na mashtaka ya kujaribu kuipindua serikali na kutatiza amani ya rais Yoweri Museveni.

Vituo hivyo vimefunguliwa hivi majuzi baada ya kufungwa kwa mda wa mwezi mmoja.

-Ripoti imeandikwa na Kennes Bwire

XS
SM
MD
LG