Waandishi wa habari nchini Sudan wameunda muungano wao, ambao ni wa kwanza, kuwahi kuundwa kwa muda wa miongo kadhaa.
Mwandishi wa shirika la habari la AFP amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa muungano huo wa waandishi wa habari.
Makundi ya wataalamu nchini Sudan yaliongoza maandamano yaliyopelekea kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa zamani wa muda mrefu Omar Al Bashir, mwaka 2019.
Waandishi wa habari wenye ushirikiano na uliokuwa utawala wa Bashir, wamejaribu kuzuia uchaguzi wa viongozi wa waandishi wa habari, uliofanyika jumapili, wakisema kwamba muungano mpya hauna uwezo wa kuchukua nafasi ya muungano uliokuwepo na uliokuwa unadhibitiwa na rais wa zamani Bashir, wakati wa utawala wake wa miaka 30.