Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 11:39

Waandishi habari wa Tanzania wadai usalama wanapofanya kazi


Waandishi wa habari waandamana jijini Dar es Salaam kudai usalama zaidi wanapofanya kazi.
Waandishi wa habari waandamana jijini Dar es Salaam kudai usalama zaidi wanapofanya kazi.
Waandishi wa habari kutoka sehemu mbali mbali za Tanzania wameandamana Jumanne mjini Dar es Salaam kuelezea masikitiko yao na kulaani mauwaji ya kikatili ya mwandishi habari mwenzao Daudi Mwangosi aliyeuwawa mapema mwezi huu katika kijiji cha Nyololo Mufini, mkoani Iringa, akiwa kazini.


Katika matamko yao mbali mbali wanahabari hao wamezitaka mamlaka za usalama nchini Tanzania kuwahakikishia usalama wanapokuwa kazini kwani moja ya majukumu yao ni kuwapatia habari wananchi na kuhakikisha misingi ya demokrasia, haki na uwajibikaji inaheshimiwa.
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:06 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mwandishi wa Sauti ya Amerika Dar es Salaam Dinah Chahali anaripoti kwamba maandamano hayo yaliyoandaliwa na Jukwa la Wahariri yalianzia kutoka kituo cha televisheni cha Channel 10 alipokuwa akifaniya kazi marhemu Mwangosi mpaka viwanja vya Jangwani

Nevil Meena Katibu Mkuu wa Jukwa la Wahariri anasema anawaomba wale wanaofikiria walipofanya maandamano yao walikosea basi anataka wafikiriye kuna madaraka makubwa sana kuliko maandamano .
XS
SM
MD
LG