Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 26, 2020 Local time: 16:07

Waandamanaji wazidi kushambuliwa Syria


Balozi wa Marekani nchini Syria Robert Ford

Vikosi vya usalama vya Syria vyazidi kushambulia raia katika maandamano.

Wanaharakati wa Syria wanasema vikosi vya usalama vimevamia mji wa Damascus kusitisha mgomo ulioanzishwa usiku wa alhamisi , kabla ya maandamano makubwa ya kumpinga rais wa Syria Bashar al- Assad yaliyopangwa kufanyika ijumaa.

Wanaharakati walisema alhamisi kwamba vikosi vya usalama vilifyatulia risasi raia walioshiriki katika maandamano hayo ya usiku. Kuna ripoti za vifo vya raia, majeruhi, na wengine kukamatwa.

Ghasia hizo zilizuka baada ya Syria kumshutumu balozi wa Marekani Robert Ford kutembelea mji wa Hama wenye upinzani mkubwa.

Wizara ya mambo ya nje ya Syria ilisema balozi huyo wa Marekani kutembelea Hama bila kibali inaonesha wazi kwamba Marekani inajaribu kuongeza mvutano na kuharibu usalama na uthabiti wa Syria.

Mjini Washington msemaji wa wizara ya mambo ya nje Victoria Nuland alisema Ford alikutana na dazani za watu katiza ziara iliyotaka kuonesha umoja na waandamanaji.

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG