Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 19:20

Waandamanaji wakusanyika kumuunga mkono Julius Malema.


Kiongozi wa vijana wa ANC Bw. Julius Malema.
Kiongozi wa vijana wa ANC Bw. Julius Malema.

Waandamanaji wakusanyika kumuunga mkono Julius Malema.

Waandamanaji walikusanyika katika makao makuu ya ya chama tawala cha Afrika kusini leo kumuunga mkono Julius Malema kiongozi mwenye matata wa chama hicho kwa upande wa vijana.

Chama cha African National Congress kinafanya siku ya pili ya kusikilizwa kesi ya utovu wa nidhamu dhidi ya Malema ambaye anashutumiwa kwa kugawa chama na kuharibu heshima ya chama hicho kwa mfululizo wa maneno makali.

Polisi wa kutuliza fujo walisimama nje ya makao makuu ya ANC huko Johanesburg katika juhudi za kuzuia kujirudia tena kwa ghasia za Jumanne katika siku ya kwanza ya kesi hiyo.

Polisi mmoja na waandishi watano walijeruhiwa wakati maelfu ya wafuasi wa Malema walipopambana na Polisi.

XS
SM
MD
LG