Waandamanaji walikabiliana na ujumbe wa upinzani nchini Syria nje ya makao makuu ya umoja wa nchi za kiarabu huko Cairo hii leo.
Baadhi ya waandamanaji wamewaita wapinzani kuwa ni wasaliti na kuwatupia mayai.
Waandishi wa habari wanasema inaonekana kama waandamanaji wana hofu kuwa viongozi wa upinzani wanaweza kukubali kufanya majadiliano na wakuu wa Syria.
Tukio hilo liliwalazimisha wajumbe wa watu wanne kuahirisha mkutano wao na maafisa wa umoja wa nchi za kiarabu mpaka baadae leo.
Walikuwa wajadili kuhusu ukandamizaji unaondelea huko Syria dhidi ya waandamanaji wanaoipinga Serikali.
Wakati huo huo Wanaharakati wanasema watu 110 wameuwawa wiki hii tangu Syria itangaze kua imekubaliana na mpango nchi za kiarabu.
Ujumbe wa Baraza la Mpito la Syria ulikua na mkutano na Umoja wa nchi za Kiarabu kujadili hatua za kuchukuliwa huko Syria, lakini walizuiliwa na waandamanaji mjini Cairo.