Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Agosti 13, 2026 Local time: 09:21

Waandamanaji wa upinzani wapambana na vikosi vya usalama

Dazeni ya waandamanaji walipambana na vikosi vya usalama katika mji mkuu wa Senegal, Dakar, Jumatatu baada ya wabunge na wafuasi wao kuzuiwa kutembelea nyumba ya kiongozi maarufu wa upinzani ambaye ana mashitaka ya ubakaji na kukashifu.

Polisi walifyatua gesi za kutoa machozi kwa waandamanaji ambao waliweka vizuizi katika moja ya barabara kuu za Dakar, na katika kitongoji kimoja walichoma gari na kuwasha moto kwenye jengo la wizara.

Ni tukio la sasa kabisa katika miezi kadhaa ya kutokuwepo na utulivu kulikosababishwa na rais Mcky Sall kukataa kutogombea muhula wa tatu na uwepo wa kesi mahakamani zinazo muhusu mpinzani wake Ousmane Sonko.

Hata hivyo Sonko, amepinga shutuma zinazo mkabili akisema zinania ya kumuondoa asigombanie urais katika uchaguzi ujao wa mwezi Febuari.

This item is part of

Forum

XS
SM
MD
LG