Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 11:52

Waandamanaji Ufaransa wamechoma majengo na kupambana na polisi


Polisi walifyatua gesi ya kutoa machozi na mipira ya maji ya moto kuwasambaratisha waandamanaji ambapo baadhi yao waliwarushia mawe polisi wa kutuliza ghasia

Waandamanaji wanaovalia fulana za njano maarufu Yellow Vest huko Ufaransa walichoma moto tawi moja la benki na kuvunja maduka mjini Paris siku ya Jumamosi wakati maandamano yao ya kuipinga serikali yalipoingia mwezi wa nne.

Tawi la benki ya Bangue Tarneaud liliwaka moto kabla ya wafanyakazi wa zimamoto kuwasili kwenye eneo na vituo viwili vya habari vilishika moto wakati moto mkubwa ulipowashwa mitaani. Polisi walifyatua gesi ya kutoa machozi na mipira ya maji ya moto kuwasambaratisha waandamanaji ambapo baadhi ya waandamanaji waliwarushia mawe polisi wa kutuliza ghasia na kuwasha magari moto mbele ya eneo lenye mnara maarufu mjini Paris la Arc de Triomphe.

Polisi waliwakamata zaidi ya waandamanaji 80 hadi saa za mchana kwa huko wakati waandamanaji walipovunja maduka kuzunguka mtaa wa Champs Elysees na kuvamia mgahawa wa kifahari wa Fouquet.

XS
SM
MD
LG