Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 07:54

Waalimu Tanzania kufanya mgomo nchi nzima.


umati wa watanzania
umati wa watanzania

wamesema waliomba kukaa meza moja na viongozi wa serikali ili kujaribu kupata suluhu ya madai yao lakini juhudi zao zimegonga mwamba.

Waalimu nchini Tanzania wameanza kupiga kura itakayowawezesha kufanya mgomo nchi nzima wa kudai nyongeza ya mishahara na posho ya mazingira magumu.

Kaimu katibu mkuu wa chama cha waalimu nchini Tanzania bwana Ezekia Oluochi amesema hivi sasa waalimu wanalipwa takriban kiasi cha silingi 244,000 ikilinganishwa na karibu shilingi 400,000 wanazotakiwa kulipwa kwa mwezi kila mmoja.

Amesema waliomba kukaa meza moja na viongozi wa serikali ili kujaribu kupata suluhu ya madai yao lakini juhudi zao zimegonga mwamba. Harakati za madai ya waalimu zilianza tangu mwaka jana ambapo walitegemea kwamba katika bajeti ya mwaka huu pengine madai yao yangeweza kufikiriwa.

Kura ya maoni ya waalimu ilianza kupigwa jumatano na itafanyika hadi ijumaa ambapo muafaka wa kutangaza mgomo huo utajulikana baada ya kura hiyo.

Amesema sheria ya Tanzania iko wazi kwamba kama mfanyakazi anashindwa kuelewana na mwajiri wake ana haki ya kufanya mgomo. Ameongeza kuwa ni jukumu la serikali kutilia uzito suala hili la madai ya waalimu hasa ikizingatiwa kwamba waalimu wanafanya kazi muda mrefu kuliko wafanyakazi wengine.

XS
SM
MD
LG