Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 23:49

Wa-Repuplican waidhinisha muongozo wa kampeni


Mitt Romney, mgombea nafasi wa kiti cha Rais kwa chama cha Repuplican

Muongozo wa chama unatoa wito pia kufanyika mabadiliko ya katiba yatakayo mpatia mtoto ambae bado hajazaliwa haki msingi ya kuishi

Wa-Repuplican wanajiandaa kwa mkutano mkuu wa chama wiki ijayo wameidhinisha muongozo au taarifa ya imani zao inayojumuisha wito wa kaufanya mabadiliko ya katiba kupiga marufuku utoaji wa mimba.

Ahadi ya chama kupinga utoaji mimba haihusishi kesi maalum za ubakaji au kujamiiana kwa mtu katika familia na ndugu wa karibu na hivyo kutofautiana na mawazo ya mgombea kiti cha Rais wa Repuplican Mitt Romney.

Muongozo wa chama unatoa wito pia kufanyika mabadiliko ya katiba yatakayo mpatia mtoto ambae bado hajazaliwa haki msingi ya kuishi ambayo haiwezi kuvunjwa. Wagombea hawahitajiki kuunga mkono muongozo au taarifa ya imani ya chama chao.

Muongozo uliidhinishwa Jumanne, siku ambayo mbunge wa chama cha Repuplican Todd Akin alipotangaza kuwa ataendelea na kinyang’anyiro cha kugombania kiti cha seneta katika jimbo la Missouri.

Akin anakosolewa vikali na wanachama wenzake kwa matamshi yake aliyoyatoa mwanzoni mwa wiki hii kwamba “ubakaji halali” haupelekei mwanamke kupata ujauzito usiotarajiwa.

Viongozi wengi wa chama cha Repuplican akiwemo Romney mwenyewe wanamtaka Akin ajiondowe kutoka kinyang’anyiro hicho wakihofia utata wa matamshi yake unaweza kuhatarisha nafasi za chama kuchukua udhibiti wa baraza la Senet bungeni .

Romney na mgombea mwenza wake Paul Ryan watateuliwa rasmi wiki ijayo kwenye mkutano mkuu wa kitaifa huko Tampa, Frolida. Takwimu za karibuni zinaonesha kampeni ya Romney inaongoza kifedha dhidi ya kampeni ya Rais Barack Obama wa Democrat.

Kwa mujibu wa ripoti ya tume ya taifa ya uchaguzi iliyotolewa Jumatatu, Romney na wa-Repuplican walichangisha dola milioni 101 mwezi Julai ikilinganishwa na dola milioni 25 zilizochangishwa mwezi uliopita za bwana Obama na wa-Democrat.
XS
SM
MD
LG