Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 01:47

Wa-Liberia wa Marekani wapambana na Ebola kwao


Kesi za Ebola katika nchi za Guinea, Sierra Leone na Liberia kama zinavyoonekana July 24, 2014.
Kesi za Ebola katika nchi za Guinea, Sierra Leone na Liberia kama zinavyoonekana July 24, 2014.

Balozi wa Liberia nchini Marekani anasema wa-Liberia wanaoishi Marekani wanatoa ushirikiano katika kusaidia utoaji msaada kufuatia mlipuko wa virusi vya Ebola vilivyosababisha vifo nchini mwao.

Jeremiah Suluntel alisema wa-Liberia wanahamasishwa kutoa mchango wa fedha au vifaa vya madawa.

Idadi ya kesi za ugonjwa wa Ebola nchini Liberia imeongezeka kufikia kiasi cha 249 na vifo 129. Rais Ellen Johnson Sirleaf, Jumapili alitoa agizo la kufungwa takribani mipaka yote ya kuingia nchini humo.

Sulunteh alisema wa-Liberia nchini Marekani wamekuwa wakielezea wasi wasi wao kuhusu mlipuko wa Ebola. “Hivi sasa wa-Liberia wanaoishi Marekani wamekuwa wakinipigia simu muda wote wa wikiendi kuona namna wanavyoweza kutoa msaada ili kuokoa maisha ya watu wengine kutokana na janga hilo nchini Liberia. Hivyo basi kampeni ya hivi sasa ni namna tunavyoweza kupanga mikakati ya kufanikisha kusaidia watu wa Liberia”.

Sulunteh alisema kundi la Global Health Ministries lenye makao yake katika jimbo la Minnesota litasafirisha kontena la kwanza la vifaa vya madawa na vinginevyo kuelekea Liberia mwishoni mwa wiki hii, Jumamosi ya Agosti 2. “Tunawahamasisha wa-Liberia wote na marafiki wa Liberia na wote wanaoitakia mema nchi hiyo kuona namna wanavyoweza kutoa msaada wa kukusanya zana za kupambana na Ebola, alisema Sulunteh.

Alisema ubalozi wa Liberia nchini Marekani upo kwenye utaratibu wa kufungua akaunti ya benki kwa wale ambao wangependa kutoa msaada kwa njia ya fedha.

XS
SM
MD
LG