Picha za marais 43 wa zamani pamoja na rais aliyeko madarakani Marekani zilionekana kwenye televisheni katika ukumbi unaofanyika mkutano mkuu wa uteuzi wa chama cha Democratic huko Philadeplhia Jumanne usiku, kila picha ikimuonesha mwanamme ambaye amehudumu kama rais wa Marekani.
Baada ya picha ya Rais Barack Obama kukuzwa na kisha picha zote kufifia hatimaye ilimuonesha Hillary Clinton, mwanamke wa kwanza kuwahi kutokea kuteuliwa kuwania urais na moja ya vyama vikubwa vya kisiasa nchini.
Clinton alisema imekuwa siku na usiku mzuri. Ni heshima ilioje mliyonipatia. Alionekana kwa njia ya video kutoka New York na alisema wademokrat wameweka historia ya kutowazuia wanamke kusonga mbele kushika nafasi za juu kabisa. Clinton alizungumza kuhusu umuhimu wa wakati huo kwa wasichana wadogo wote ambao walikuwa wakiangalia mkutano huo. Alisema huwenda nikawa rais wa kwanza mwanamke, lakini mmoja wenu atafuatia.