Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 19:58

Vyama vya wafanyakazi Nigeria vinasema mgomo utaendelea


Waandamanaji wakinadamana huko Nigeria baada ya ruzuku ya bei ya mafuta kuondolewa.. (AP Photo/Sunday Alamba)
Waandamanaji wakinadamana huko Nigeria baada ya ruzuku ya bei ya mafuta kuondolewa.. (AP Photo/Sunday Alamba)

Wanigeria wanakimbilia madukani kwa wasi wasi unaotokana na mgomo na kukuta bei ziko juu huku vyma vya wafanyakazi vikidai mgomo utaendelea.

Vyama vya wafanyakazi vya Nigeria vinasema mgomo wa nchi nzima utaendelea jumatatu baada ya mazungumzo na serikali juu ya bei za mafuta ya petroli kushindikana.

Wawakilishi wa vyama hivyo pia walitangaza wamesitisha kitisho cha awali kusimamisha uzalishaji mafuta.

Wakati wa mazungumzo Jumamosi viongozi wa vyama vya wafanyakazi wameitaka serikali kurudisha bei za mafuta ya petroli kama ilivyokuwa kabla ya dola bilioni 8 kuondolewa katika ruzuku ya mafuta mwanzoni mwa mwezi huu. Baada ya saa kadhaa za mvutano pande hizo mbili zilimaliza mazungumzo bila makubaliano.

Raundi nyingine ya mazungumzo ilikuwa ikitazamiwa kuanza jumapili.

Kwa hivi sasa wanigeria wamekuwa wakikimbilia madukani na sokoni ili kujaza vyakula na kukuta bei zimepanda mno katika baadhi ya maeneo kufikia hadi mara tatu.

XS
SM
MD
LG