Ili kukabiliana naye kwenye uchaguzi huo, vyama 26 vya upinzani vimeungana wiki hii kikiwemo kile kikuu cha Congress Party pamoja na vyama vingine vya kieneo kutoka kwenye majimbo kadhaa nchini humo.
Muungano wa vyama hivyo umepewa jina INDIA likiwa na maana ya India National Developmental inclusive Alliance. Kiongozi wa chama cha upinzani cha Congress Rahul Gandhi, amesema kwamba ushindani wa mwaka ujao ni kati ya muungano wao wa INDIA na waziri mkuu Narendra Modi.
Rahul Verma kutoka kituo cha Sera na Utafiti mjini New Delhi amesema kwamba vyama vya upinzani vinahisi kwamba haviwezi kukishinda chama cha Modi iwapo havitaungana kwenye uchaguzi ujao. Tawkimu za 2019 zilionyesha chama cha Modi kikiwa asilimia 37 ya kura, wakati vyama vingine vikiwa na asilimia 63 ya kura.
Forum