Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 03:53

Vyama vya upinzani vya Afrika Kusini kuunda muungano wa kuondoa ANC madarakani


Wajumbe wakiwasili kwenye kongamano la 55 la chama cha ANC mjini Johannesburg, Africa Kusini. Decemba 16, 2022.
Wajumbe wakiwasili kwenye kongamano la 55 la chama cha ANC mjini Johannesburg, Africa Kusini. Decemba 16, 2022.

Vyama 7 vya kisiasa vya Afrika Kusini Alhamisi vimefikia makubaliano ya kuunda muungano wa kuondoa chama tawala cha ANC madarakani, iwapo hakitapata wingi wa viti kwenye uchaguzi mkuu mwaka ujao.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, miongoni mwa vyama hivyo ni chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance, pamoja na vingine, vikiwa vimekubaliana kwa kile vimetaja kuwa Multi-Party Charter for South Africa.

Makubaliano hayo yamefanyika siku mbili baada ya siku mbili za mkutano huko Kempton Park mashariki mwa Johannesburg. ANC ndicho chama cha marehemu Nelson Mandela, na ifikapo mwaka ujao, kitakuwa madarakani kwa miaka 30 tangu taifa hilo kujipatia uhuru wake.

Chama hicho kiliongoza vuguvugu dhidi ya ubaguzi wa rangi, na hatimaye kikachukua usukani wa Afrika Kusini kufuatia uchaguzi mkuu wa 1994, ambapo Nelson Mandela alichaguliwa kuwa rais.

Hata hivyo umaarufu wa chama hicho umeendelea kushuka, wakati kikilaumiwa kwa kushindwa kutoa huduma muhimu pamoja na kuatokomeza umaskini miongoni mwa watu weusi ambao ndio wengi Afrika Kusini.

Forum

XS
SM
MD
LG