Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 12:55

Vyama vya siasa Sudan vyaanza mazungumzo ya mwisho kuunda serikali ya kiraia

Mkuu wa Jeshi la Sudan Jenerali Abdel-Fattah Burhan akizungumza kufuatia kutiwa saini kwa makubaliano ya awali yenye lengo la kumaliza mgogoro mkubwa uliosababishwa na mapinduzi ya kijeshi ya mwaka jana, mjini Khartoum, Sudan, Jumatatu, Desemba 5, 2022.

Vyama vya siasa nchini Sudan vilianza mazungumzo Jumatatu kujaribu kufikia makubaliano ya mwisho ya kuunda serikali ya kiraia na kutatua masuala mengine ambayo bado hayajakamilika zaidi ya mwaka mmoja baada ya mapinduzi ya kijeshi.

Mwezi uliopita, vyama hivyo vilitia saini mkataba na jeshi ili kuanzisha mageuzi mapya ya kisiasa kuelekea uchaguzi, lakini waandamanaji walikosoa makubaliano hayo kuwa hayana uwakilishi, na yaliacha mambo yenye utata kwa ajili ya mazungumzo zaidi.

Moja ya hoja hizo, sera ya kuuvunja utawala wa Omar al-Bashir baada ya kupinduliwa kufuatia uasi wa mwaka 2019, ni ya kwanza kushughulikiwa katika mazungumzo wiki hii.

The process of dissolving Bashir-era institutions and retrieving funds was one source of tension between political leaders and the military in the run-up to the October 2021 coup.

Mchakato wa kufuta taasisi za enzi za Bashir na kurejesha fedha kilikuwa chanzo cha mivutano kati ya viongozi wa kisiasa na jeshi katika kuelekea mapinduzi ya Oktoba 2021.

XS
SM
MD
LG