Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 04:21

Vuguvugu la Polisario linakutana Sahara Magharibi kufanya uchaguzi


Vuguvugu la Polisario linalodai uhuru katika eneo linalozozaniwa la Sahara Magharibi
Vuguvugu la Polisario linalodai uhuru katika eneo linalozozaniwa la Sahara Magharibi

Zaidi ya wanachama 2,200 wa vuguvugu hilo na wageni 370 wanahudhuria mkutano huo wa siku tano katika jangwa la Algeria kwenye  kambi ya wakimbizi ya Sahrawi iliyopewa jina la Dakhla mji wa bandari wa Atlantiki katika eneo la Sahara Magharibi linalodhibitiwa na Morocco

Vuguvugu la Polisario ambalo linadai uhuru katika eneo linalozozaniwa la Sahara Magharibi linakutana Ijumaa kwa ajili ya uchaguzi wa uongozi kivuli huku mivutano ikiongezeka kati ya wenyeji Algeria na Morocco ambapo wanadhibiti sehemu kubwa ya eneo hilo.

Zaidi ya wanachama 2,200 wa vuguvugu hilo na wageni 370 wanahudhuria mkutano huo wa siku tano katika jangwa la Algeria kwenye kambi ya wakimbizi ya Sahrawi iliyopewa jina la Dakhla mji wa bandari wa Atlantiki katika eneo la Sahara Magharibi linalodhibitiwa na Morocco.

Kiongozi wa sasa wa Polisario, Brahim Ghali mwenye umri wa miaka 73 anaonekana kufurahia uungwaji mkono muhimu wa Algeria na anatarajiwa kuchaguliwa tena katika mkutano huo ambao unakuja wakati muhimu kwa harakati hizo.

"Ni mkutano wa kwanza tangu mapambano ya silaha yaanze tena," mwakilishi wa vuguvugu hilo nchini Afrika Kusini, Islam Beissat aliliambia shirika la habari la AFP.

XS
SM
MD
LG