Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 17:31

Sudan: Mapigano mapya yatishia utulivu ambao ulianza kushuhudiwa


Mgogoro wa Sudan umewasukuma wakimbizi wa Sudan Kusini kurejea katika matatizo nchini Sudan Kusini, jambo ambalo hawajalifurahia.
Mgogoro wa Sudan umewasukuma wakimbizi wa Sudan Kusini kurejea katika matatizo nchini Sudan Kusini, jambo ambalo hawajalifurahia.

Mapigano ya hapa na pale kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha jeshi la dharura RSF, yameendelea mjini Khartoum na kuvuruga hali ya utulivu ambao ulikuwa umeanza kushuhudiwa wiki hii.

Mapigano hayo yamesababisha wasiwasi wa kuongezeka kwa hali mbaya ya kibinadamu.

Makubaliano ya kusitisha vita, ambayo yanafuatiliwa na Saudi Arabia pamoja na Marekani, yalipatikana baada ya wiki tano za mapigano mjini Khartoum na sehemu nyingine za Sudan, ikiwemo katika eneo la Darfur ambalo limeshuhudia ukosefu wa amani kwa muda mrefu.

Mapigano ya Sudan yanahusu mgogoro wa madaraka kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha jeshi la dharura RSF.

Yamepelekea kuwepo hali mbaya ya kibinadamu, na zaidi ya watu milioni 1 laki 3 kuhama makwao, pamoja na kuyumbisha usalama wa eneo hilo lenye misukosuko.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema kwamba kuna ukiukwaji wa makubaliano ya kusitisha vita, ikiwemo matumizi ya ndege za kivita, silaha na ndege zisizokuwa na rubani.

Marekani imeonya kwamba kundi la mamluki wa Russia, Wagner, limekuwa likitoa silaha ikiwemo makombora ya anga, kwa kikosi cha RSF kupigana na jeshi la Sudan na kusababisha mapigano kuendelea.

Forum

XS
SM
MD
LG