Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 05:29

Vituo vya kupiga kura Marekani vimeanza kufungwa


Wapiga kura katika eneo la Fernald jimbo la Iowa, Nov. 8, 2016.

Wagombea urais wa Marekani na wagombea wenza wao walipiga kura zao mapema Jumanne wakiungana na mamilioni ya wamarekani katika moja ya uchaguzi unaoelezewa wa kipekee katika historia ya karibuni.

Mgombea mwenza wa Democratic, Tim Kaine alikuwa wa kwanza kupiga kura yake akiwa pamoja na mkewe Ann Holton nyumbani kwake Richmond, katika jimbo la Virginia. Kaine aliwaambia waandishi wa habari kuwa alikuwa akipiga kura katika eneo hilo kwa takriban miaka 24 na anajisikia vizuri kuweza kutembea kutoka nyumbani kwake.

Mgombea mwenza wa Trump, gavana wa jimbo la Indiana, Mike Pence hakwenda mbali kupiga kura alikuwa amefuatana na mkewe Karen pamoja na binti yake aitwaye Charlotte walivuka barabara kutoka kwenye makazi ya gavana na kwenda kupiga kura kwenye kanisa la St. Thomas Aquinas.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG